18.4 C
New York

Baada ya Ederson, Carrick ataka ‘mido’ mwingine

Published:

MANCHESTER, Uingereza

MANCHESTER United imekamilisha usajili wa Ederson kutoka Atalanta ya Serie A, kocha Michael Carrick ametaka kiungo mwingine wakati huu wa dirisha kubwa la kiangazi.

Nyota huyo raia wa Brazil atatua Old Trafford kwa mkataba wa miaka minne baada ya Man United kuipatia Atalanta kiasi cha euro milioni 40.

Ka upande wake, Carrick anaamini bado anahitaji kiungo mmoja kwa kuwa Manuel Ugarte na Casemiro wataondoka klabuni hapo.

Carrick amepewa mkataba wa miaka miwili kuliongoza benchi la ufundi la Man United baada ya kufanya vizuri msimu uliomalizika hivi karibuni.

Licha ya kuikuta Man United ikiwa kwenye hali mbaya, aliiongoza timu hiyo kumaliza ndani ya ‘Top 4’ na kukata tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Related articles

Recent articles