MADRID, Hispania
Kiungo wa Manchester City, Rodrigo Hernández, amesema kwa sasa anaelekeza akili yake kwenye fainali za Kombe la Dunia, licha ya kuzisikia tetesi za kutakiwa Real Madrid.
Mhispania huyo ameeleza kuwa atafanya uamuzi wa hatima yake baada ya kumalizika kwa michuano hiyo ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
“Tuko hapa kuzungumzia Kombe la Dunia. Lolote linalohusu hatima yangu nitalizungumzia baada ya Kombe la Dunia,” amesema.
Wakati huo, nyota huyo kwenye umri wa miaka 29 atakuwa amebakiza chini ya mwaka mmoja katika mkataba wake na Man City.
Mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu ujao wa klabu ya Madrid, Enrique Riquelme, ameahidi kumsajili Rodri endapo atachaguliwa.


