20.5 C
New York

Arteta kulamba mkataba mpya Arsenal

Published:

LONDON, Uingereza

MABOSI wa Arsenal wanataka kumpa mkataba mpya kocha wao raia wa Hispania, Mikel Arteta, kabla ya timu hiyo kuanza kambi ya ‘pre-season’.

Haraka hiyo ya uongozi inatokana na mafanikio makubwa ya Arsenal chini ya Arteta, ambapo ameipa ubingwa wa Ligi Kuu baada ya miaka 22, pia akiifikisha fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kwa upande wake, Arteta hajaonesha nia ya kuondoka Emirates, hivyo anasubiri kuona ofa atakayowekewa mezani hivi karibuni.

Kwa mujibu wa ripoti, tayari kuna mazungumzo ya mkataba mpya yanayoendelea kati ya Arteta na Mkurugenzi wa Michezo wa Arsenal, Andrea Berta.

Aidha, taarifa ambazo hazijathibitishwa na Arsenal wala Arteta ni kwamba kocha huyo atapewa mkataba wa miaka mitatu, ukiwa na ongezeko kubwa la mshahara wake.

Related articles

Recent articles