19.8 C
New York

Wilshere awashusha presha mashabiki Arsenal

Published:

LONDON, Uingereza

KIUNGO wa zamani wa Arsenal, Jack Wilshere, anaamini klabu hiyo haitosubiri tena miaka 20 kufika fainali na kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kauli ya Wilshere imekuja kuwapoza mashabiki wa Arsenal, ambao usiku wa jana Mei 30, 2026 waliishuhudia timu yao ikipoteza fainali ya michuano hiyo kwa kufungwa kwa penalti 4-3 na PSG.

Washika Bunduki walionekana wangeshinda mechi hiyo baada ya Kai Harvetz kuifungia bao la mapema katika dakika ya tano tu ya mchezo huo uliochezwa Budapest, Hungary.

Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko, Washika Bunduki walikuwa mbele kwa bao 1-0, kabla ya Ousmane Dembele kuisawazishia PSG kipindi cha pili, dakika ya 64.

“itawachukua muda kurudi na kuwa sawa lakini naamini haitawachukua tena miaka 20 kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa wakiwa na (Mikel) Arteta kwenye benchi,” alisema Wilshere.

Naye kiungo wa zamani wa Manchester United, Owen Hargreaves, ameitaja Arsenal kuwa ndiyo timu bora zaidi kwa sasa Ligi Kuu ya England na Ulaya kwa ujumla, licha ya kufungwa na PSG.

Related articles

Recent articles