17.4 C
New York

Hivi ndivyo Chelsea walivyoteseka 2025-26

Published:

LONDON, Uingereza

BLUES waliuingia msimu huu wakiwa na ‘mzuka’ baada ya kutwaa mataji makubwa mawili; Ligi ya Europa na Kombe la Dunia kwa ngazi ya Klabu. Miezi tisa baadaye, mambo ni tofauti.

Wamemaliza mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) wakiwa hawana tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao baada ya kushika nafasi ya 10 kwenye msimamo.

Katika Kombe la FA, walifika fainali na kupoteza. Kwa upande wa EFL Cup, waliishia nusu fainali. Kwa Ligi ya Mabingwa, walikwamia hatua ya 16 Bora. Hakuna taji lolote mkononi.

Wakati wakiwa na mabao ya kufunga 109 katika mechi za michuano mbalimbali waliyoshiriki, safu ya ulinzi imeruhusu kutikiswa mara 83.

Nyota raia wa Brazil, Joao Pedro, ndiye aliyemaliza akiwa mfungaji bora wa kikosi chao. Mabao 20, huku 15 kati ya hayo akifunga katika mechi za EPL.

Pedro aliziona nyavu mara mbili pekee kwenye mechi zake nane za Ligi ya Mabingwa, pia alifunga mabao mawili pekee katika mechi zake 11 za mwisho wa msimu.

Nyota mwingine aliyekuwa na msaada mkubwa kwa Chelsea ni Enzo Fernandez, ambaye alichangia mabao 22, akifunga 15 na kutoa ‘asisti’ saba.

Msimu ujao, Blues watakuwa chini ya kocha raia wa Hispania, Xabi Alonso, ambaye anatarajiwa kuanza kazi Juni Mosi, 2026.

Je, kocha huyo wa zamani wa Real Sociedad, Bayern Leverkusen na Real Madrid atairejesha Blues katika ubora wake wa misimu kadhaa iliyopita?

Related articles

Recent articles