14.4 C
New York

Barca kumlipa Gordon mshahara wa bil. 21.4/-

Published:

CATALUNYA, Hispania

WINGA wa kimataifa wa England, Anthony Gordon, amejiunga na Barcelona na mshahara wake ni euro milioni saba (zaidi ya Sh bil. 21.4 za Tanzania) kwa mwaka.

Nyota huyo aliyetokea Newcastle United amesaini mkataba wa miaka mitano, akizitupilia mbali ofa za Arsenal na Bayern Munich zilizokuwa zikimtolea macho.

Barcelona wameinasa saini yake baada ya kuipa Newcastle kiasi cha euro milioni 80, ambapo itaongeza 10 endapo ataonesha kiwango kizuri akiwa Camp Nou.

Nje ya mshahara, Gordon atakuwa akivuna posho ya euro milioni tano kutokana na mchango wake kikosini.

Kwa upande wao, Newcastle watakuwa wakipokea euro milioni moja kwa kila msimu ambao Gordon atacheza zaidi ya asilimia 60 ya mechi.

Aidha, klabu yake ya zamani ya Everton iliweka kipengele cha kupewa asilimia 15 katika kila usajili wa mchezaji huyo.

Ni kwa maana hiyo, klabu hiyo ya mjini Merseyside itavuna euro milioni 12 kutoka katika dau walipopata Newcastle kutoka kwa mabosi wa Barcelona.

Related articles

Recent articles