MERSEYSIDE, Uingereza
KLABU ya Aston Villa imejitosa katika mbio za kuiwania huduma ya kiungo wa Liverpool raia wa England, Joe Gomez.
Baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Europa na kukata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, kocha Unai Emery ameanza kuimarisha kikosi chake cha msimu ujao.
Emery anatajwa kuwa ni shabiki mkubwa wa mchezaji huyo kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi nyingi uwanjani.
Mkataba wa Gomez na Liverpool utafikia ukomo mwaka 2027 lakini amekuwa akihusishwa na mpango wa kuondoka majira ya kiangazi, 2026.
Msimu huu, nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 amecheza mechi 33 za mashindano yote, ambapo 17 alitokea benchi.
Aidha, huu ni mwaka wake wa 11 akiwa na Liverpool, akicheza mechi 274 za michuano mbalimbali.


