CATALUNYA, Hispania
KLABU ya Barcelona imeripotiwa kuingia kwenye hatua za mwisho za kumsajili winga wa Newcastle United, Anthony Gordon, ambaye pia anazitoa udenda Arsenal na Bayern Munich.
Hiyo ni kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo maarufu wa Italia, ambaye anasifika kwa usahihi wa taarifa za usajili, Fabrizio Romano.
Romano amedai kuwa Mkurugenzi wa Michezo wa Barcelona, Deco, ameshawasili jijini London kushughulikia dili hilo.
“Barcelona wako kwenye mazungumzo ya moja kwa moja na klabu ya Newcastle kuzungumzia dili la Anthony Gordon,” amesema Romano.
Kwa upande wake, Newcastle wako tayari kumuuza nyota wao huyo endapo tu watawekewa mezani Pauni milioni 100.


