LONDON, Uingereza
MKONGWE wa Ligi Kuu ya England (EPL), Paul Merson, amemtaka kocha mpya wa Chelsea, Xabi Alonso, kumrudisha kikosini straika Nicolas Jackson.
Baada ya kushindwa kung’ara Chelsea, Jackson alipelekwa kwa mkopo Bayern Munich, ambako ameweza kucheza kwa kiwango cha juu, hasa msimu wa 2025-26 uliomalizika hivi karibuni.
Kwa upande wake, Merson anaamini Chelsea ya sasa haina straika wa kiwango cha nyota huyo wa kimataifa wa Senegal.
“Chelsea walihitaji kocha wa viwango, tayari wanaye Xabi Alonso. Sasa wanahitaji wachezaji. Kama ningekuwa mimi, ningemrejesha Jackson,” amesema Merson.
Alonso, baada ya kutimuliwa Real Madrid miezi michache iliyopita, ataanza majukumu yake mapya Stamford Bridge ifikapo Juni Mosi, 2026.


