25.8 C
New York

Mabosi United wamrudisha mezani Bruno

Published:

MANCHESTER, Uingereza

UONGOZI wa Manchester United umesitisha mpango wake wa kumpiga bei Bruno Fernandes baada ya kiwango kizuri alichokionesha kiungo huyo raia wa Ureno msimu huu wa 2025-26.

Bruno amemaliza msimu akiwa na tuzo kubwa mbili; Mchezaji Bora wa Mwaka wa Chama cha Waandishi wa Habari za Soka nchini England (FWA) na Mchezaji Bora wa Mwaka wa Ligi Kuu.

Hivyo, mabosi wa Man United wameamua kuanzisha mazungumzo ya kumpa mkataba mnono ili kuzuia uwezekano wa klabu za Saudi Arabia kumsajili.

Mkataba wake na Man United utakwisha Juni, 2027 na tayari alishaonesha nia ya kuondoka Old Trafford tangu aliposema baadhi ya viongozi hawamtaki.

Katika mkataba wake wa sasa, kuna kipengele kinachomruhusu ‘mido’ huyo mwenye umri wa miaka 31 kusajiliwa na klabu nyingine kwa Pauni milioni 57.

Related articles

Recent articles