LONDON, Uingereza
ALIPOTEULIWA kuinoa Tottenham, kocha Roberto De Zerbi alikiri wazi mbele ya waandishi wa habari, kwamba ana bahati mbaya kuajiriwa wakati ambao timu timu hiyo inateswa na wimbi la majeraha kwa wachezaji wake muhimu.
Hivi karibuni, mshambuliaji wake, Xavi Simons, alipata majeraha yatakayomuweka nje ya uwanja hadi msimu ujao. Pia, atazikosa fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu.
Simons anaunga na wachezaji wengi muhimu wa Tottenham wanaouguza majeraha, sababu inayotajwa kuchangia mwenendo mbovu wa timu hiyo msimu huu.
Dominic Solanke: Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 alipata majeraha ya nyama za paja katika mchezo wao dhidi ya Wolves na amekuwa nje ya uwanja tangu Aprili 25, 2026.
Xavi Simons: Aliumia goti Aprili 25, 2026, wakati Tottenham ikikabiliana na Wolves, mchezo ambao Tottenham ilipata ushindi.
Cristian Romero: Mara yake ya mwisho kwa Muargentina huyo kucheza ilikuwa Aprili 12, 2026, mechi dhidi ya Sunderland. Aliumia goti katika mchezo huo.
Wilson Odobert: Hajaonekana uwanjani tangu Februari 10, 2026, katika mchezo dhidi ya Newcastle United. Aliumia goti na kukosekana kwake ni pigo kubwa kwa Tottenham.
Ben Davies: Beki huyo alipata majeraha Januari 17, 2026, wakati Tottenham ikicheza dhidi ya West Ham United. Ni wazi Davies atamaliza msimu akiwa nje ya dimba.
Mohammed Kudus: Maumivu ya nyama za paja yamemuweka nje ya dimba tangu Januari 4, 2026, katika mechi dhidi ya Sunderland. Atazikosa fainali zijazo za Kombe la Dunia.
Dejan Kulusevski: Hajacheza tangu Mei, 2025. Alipata majeraha ya goti katika mchezo dhidi ya Crystal Palace. Hata hivyo, huenda akaziwahi fainali zijazo za Kombe la Dunia.


