LONDON, Uingereza
LEJENDARI wa Ligi Kuu ya England (EPL), Rio Ferdinand, amesema kama si Michael Carrick, basi Luis Enrique wa PSG ndiye kocha sahihi wa kukabidhiwa mikoba ya kuiona Manchester United msimu ujao.
Man United imeendelea kuhusisishwa na makocha kadhaa, akiwamo Enrique, licha ya Michael Carrick kuirejesha timu hiyo kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Carrick, kiungo wa zamani wa Man United, amekuwa akieleza wazi ndoto yake ya kubaki Old Trafford kwa ajili ya msimu ujao.
Rio, kwa upande wake, amesema Carrick anapaswa kuwa kipaumbele kwa kazi aliyofanya na endapo hatopewa mkataba, basi Man United imgeukie Enrique.
Akizungumzia Enrique, amesema: “Ni kocha mkubwa. Kama anapatikana, sijali kuhusu Carrick, apewe ajira kwa kile alichokifanya PSG.”


