25.7 C
New York

Lewandowski kukipiga wapi msimu ujao?

Published:

CATALUNYA, Hispania

MSHAMBULIAJI mkongwe wa Barcelona, Robert Lewandowski, ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa Juni, 2026.

Lewandowski (37), alijiunga na Barcelona mwaka 2022 akitokea Bayern Munich na ameshawafungia Wacatalunya hao jumla ya mabao 119 na kutoa ‘asisti’ 24 katika mechi 191.

Kwa msimu huu, Lewandowski raia wa Poland ameshaingia kambani mara 18 na asisti nne katika mechi 44 za mashindano mbalimbali.

Tangu Lewandowski alipoweka wazi kuwa huu ni msimu wake wa mwisho Camp Nou, klabu kadhaa za England zimeingia vitani kuisaka saini yake.

Klabu hizo ni Manchester United, Liverpool na Chelsea, ikielezwa kuwa Juventus na Porto nazo zinampigia hesabu straika huyo wa zamani wa Borussia Dortmund.

Wakati huo huo, zipo taarifa kuwa klabu za Ligi Kuu ya Saudi Arabia na zile za Marekani, ikiwamo Chicago Fire, zinaimezea mate huduma yake.

Hata hivyo, kwa mujibu wa ripoti, Lewandowski anavutiwa zaidi na mpango wa kuendelea kucheza soka barani Ulaya, hivyo hatokwenda Saudia wala Marekani.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img