13.9 C
New York

Prisons ilivyoipa Simba bonge la rekodi

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini

KATIKA mchezo wa jana Mei 10, 2026, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Tanzania Prisons na kuweka rekodi iliyodumu klabuni hapo kwa siku 367.

Iko hivi; kabla ya kuvaana na Prisons Mei 10, 2026, Wekundu wa Msimbazi hawakuwa wamepata ushindi wa mabao manne kwenye Ligi tangu walipoifunga Pamba Jiji mabao 5-1 katika mchezo wa Mei 8, 2025.

Hivyo, ushindi wa mabao 4-0 umekuja baada ya siku 368 kupita, jambo ambalo linaweza kuashiria kuwa Simba imeanza kurudisha utamaduni wake wa kutembeza vichapo vizito kwenye Ligi.

Katika mchezo wa jana, Wekundu wa Msimbazi walipata mabao yao kupitia kwa viungo Mourice Abraham (dk. 28) na Clatous Chama (dk. 42), mshambuliaji Seleman Mwalim (dk. 44), na beki Ismail Toure (dk. 63).

Kwa upande mwingine, imekuwa mara ya kwanza kwa Prisons ‘Wajelajela’ kuruhusu mabao manne ya mchezo mmoja wa Ligi tangu ilipofungwa 4-1 na Coastal Union katika mechi iliyochezwa Februari 10, 2026.

Matokeo hayo sasa yameibakiza Simba katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara msimu huu wa 2025-26, ikibakiza pointi tano kufikia Yanga yenye 54 ikiwa kileleni.

Wakati Prisons wakiisubiri Fountain Gate katika mchezo wa Mei 13, 2026, Simba itarejea dimbani kesho yake, safari hii ikiwa ugenini mkoani Kigoma kumenyana na Mashujaa.

Kuelekea mchezo huo, rekodi zinaibeba Simba, ambayo imeshinda mechi nne za Ligi kati ya tano ilizokutana na Mashujaa hivi karibuni. Mchezo wa mzunguko kwanza msimu huu wa Ligi ulimalizika kwa Mashujaa ‘kufa’ mabao 2-0.

Aidha, amesema ndoa za utotoni na migogoro ya kifamilia pia zimekuwa chanzo cha watoto wengi kukosa mahitaji muhimu kutokana na baadhi ya wazazi kukimbia familia na kushindwa kutekeleza wajibu wao.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img