8.7 C
New York

Arsenal sasa washindwe wao tu ubingwa EPL

Published:

LONDON, Uingereza

KABLA ya kuivaa West Ham katika mchezo uliopita, Arsenal ilitabiriwa ubingwa wa Ligi Kuu na aliyekuwa beki kisiki wa Liverpool, Jamie Carragher.

“Endapo Arsenal itaifunga West Ham katika Uwanja wa London Jumapili hii, basi watatwaa ubingwa wa Ligi Kuu,” alisema Carragher.

Carragher aliyasema hayo baada ya Man City inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England (EPL) kulazimishwa sare ya mabao 3-3 na Everton.

Dhidi ya West Ham, Arsenal ilishinda bao 1-0, Leandro Trossard akiwa ndiye aliyeibuka shujaa wa Washika Bunduki baada ya bao lake lililoifanya timu hiyo kuendelea kuiacha Man City kwa pointi tano.

Unaweza kuiita siku ya bahati kwa kocha Mikel Arteta na vijana wake kwani West Ham walisawazisha dakika za majeruhi, kabla ya mwamuzi wa kati kutengua bao la Callum Wilson baada ya kujiridhisha kupitia tekonolojia ya VAR.

Pia, Arsenal walialazimika kuvuja jasho jingine uwanjani kwani West Ham haijakuwa imefungwa mbele ya mashabiki wake katika mechi sita mfululizo za Ligi Kuu.

Kabla ya mchezo huo, pengo lilikuwa ni pointi mbili tu, baada ya Man City kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Brentford katika mchezo wa juzi Mei 9, 2026.

Kwa sasa, matumaini makubwa waliyonayo mashabiki wa Arsenal ni kuiona timu yao ikitwaa kwa mara ya kwanza ubingwa wa Ligi tangu ilipofanya hivyo msimu wa 2003-04.

Mtandao maarufu wa takwimu wa Opta supercomputer kwa sasa unaipa Arsenal asilimia 87.2 ya kuwa mabingwa wapya wa Ligi msimu huu wa 2025-26.

Baada ya kazi ngumu ya kuondoka na pointi tatu za ugenini dhidi ya West Ham, Arsenal watarejea Emirates kuivaa Burnley, kabla ya kuifuata Crystal Palace. Ushindi wa mechi hizo utatosha kuipa ubingwa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img