9.5 C
New York

Slot bado yupo sana Liverpool

Published:

MERSEYSIDE, Uingereza
LIVERPOOL haina mpango wa kumfuta kazi kocha wake raia wa Uholanzi, Arne Slot, na badala yake atainoa timu hiyo msimu ujao.
Baada ya kuanza msimu wake wa kwanza (2024-25) kwa kuipa ubingwa

wa Ligi Kuu, safari hii mambo ni magumu kwa Slot, ambaye anakwenda kumaliza akiwa hana taji lolote.

Katika mchezo uliopita, Liverpool walipata ‘ushindi wa jioni’ wa mabao 2-1 dhidi ya Everton, wafungaji wakiwa ni Mohamed Salah na Virgil van Dijk aliyepasia vyavu dakika ya 100.
Taarifa zinaeleza kuwa mabosi wa Liverpool wako bega kwa bega na kocha huyo, licha ya mwenendo usioridhisha wa timu hiyo.
Hata hivyo, bado mashabiki wa Liverpool wamegawanyika, ambapo wapo wanaotaka abaki, huku wengine wakiamini anapaswa kutimuliwa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img