9.5 C
New York

Ndoto za ubingwa: Arsenal tabu iko pale pale?

Published:

LONDON, Uingereza
KICHAPO cha mabao 2-1 kutoka kwa Manchester City kimeibua hofu kubwa kwa mashabiki wa Arsenal na sasa wanaiona hatari ya timu yao kuambulia patupu msimu huu wa Ligi Kuu ya England (EPL).
Washika Bunduki hao wamebakiza tofauti ya pointi tatu pekee wakiwa na mechi tano pekee, wakati wapinzani wao wakubwa, Man City, wako nafasi ya pili na wana ‘kiporo’ kimoja (dhidi ya Crystal Palace).
Kwamba hesabu zinaweza kuwa mbaya zaidi kwa Mikel Arteta na vijana wake endapo Man City wataifunga Burnley katika mchezo wa usiku wa leo Aprili 21, 2026.
Endapo Man City watashinda, basi watalingana pointi na Arsenal, hivyo timu tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa ndiyo itakayoamua timu ya kukaa kileleni.
Kwa Man City kupoteza mchezo wa leo (dhidi ya Burnley) ni jambo linaloonekana kuwa gumu. Vijana hao wa Pep Guardiola wamefungwa mara moja pekee katika mechi 20 za EPL walizocheza hivi karibuni.
Kwa Arsenal, wanaisubiri Newcastle United wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kushinda mechi moja tu kati ya sita za hivi karibuni kwenye michuano mbalimbali.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img