9.5 C
New York

Chelsea, United zamng’ang’ania Adeyemi

Published:

LONDON, Uingereza
VIGOGO wa Ligi Kuu ya England, Chelsea na Manchester United, wamejikuta kwenye njia moja wakiiwania saini ya mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Karim Adeyemi.
Gazeti la Fussballdaten la Ujerumani limeripoti kuwa Chelsea wameanza kuwasiliana na wakala wa mchezaji huyo, Jorge Mendes.
Adeyemi mwenye umri wa miaka 24, amecheza mechi 144, akifunga mabao 35 na asisti 15 tangu alipojiunga na Dortmund mwaka 2022 akitokea Red Bull Salzburg.
Kwa msimu huu, ameshaingia kambani mara 10 na asisti tano katika mechi 37 za michuano mbalimbali.
Nyota huyo, ambaye pia anawatoa udenda mabosi wa Newcastle United, anakaribia kuingia miezi 12 ya mwisho katika mkataba wake na klabu hiyo ya Bundesliga.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img