9.5 C
New York

Mbappe achagua kocha mpya Madrid

Published:

MADRID, Hispania

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Kylian Mbappe, havutiwi na tetesi za klabu hiyo kumtaka Jurgen Klopp, na badala yake anatamani Zinedine Zidane aajiriwe.

Klopp amekuwa akihusishwa zaidi na ajira hiyo tangu Madrid ilipomfuta kazi kocha raia wa Hispania, Xabi Alonso.

Alonso, kiungo wa zamani wa Madrid, alitimuliwa Januari, 2026 na sasa timu hiyo iko chini ya kocha wa muda, Alvaro Arbeloa.

Mabosi wa Madrid wanataka kocha mpya apatikane mapema ili awahi maandalizi ya msimu ujao (pre-season).

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo maarufu wa Italia, Fabrizio Romano, uongozi wa Madrid unamtaka Klopp.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img