LONDON, Uingereza
KABLA ya mechi yao dhidi ya Manchester United kuanza, mashabiki wa Chelsea walionekana wakiandamana nje ya Uwanja wa Stamford Bridge wakishinikiza mabadiliko yanayoweza kurejesha furaha klabuni hapo.
Kelele hizo zilisikika kwa wingi pia kipindi cha pili cha mchezo huo wa Ligi Kuu uliomalizika kwa Blues kufungwa bao 1-0.
Presha ya mashabiki inatokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo, ambapo imeshafungwa mechi nne za Ligi zilizopita.
Kwa upande wake, kocha Liam Rosenior amekiri kuwa na kazi kubwa ya kufanya kuweza kupata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Kwamba sasa mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu wapo nje ya ‘Top 5’ ya msimamo kwa tofauti ya pointi nne.
Endapo itatokea, itakuwa ni mara ya tatu kwa Blues kukosa michuano hiyo katika misimu minne ya uongozi wa matajiri wapya walioinunua klabu hiyo mwaka 2022.


