MANCHESTER, Uingereza
KLABU ya Manchester City inataka kuvunja rekodi ya usajili duniani wa mchezaji wa ulinzi kwa kumchukua staa wa Newcastle United, Tino Livramento.
Man City wamepanga kumnasa kwa dau litakalomfanya Livramento kuwa beki aliyesajiliwa kwa fedha nyingi zaidi katika ulimwengu wa soka.
Kwa sasa, beki wa kulia wa PSG raia wa Morocco, Achraf Hakimi, ndiye anayeshikilia rekodi hiyo.
Hakimi alisajiliwa na PSG mwaka 2021 akitokea Inter Milan, dili hilo likitajwa kugharimu Pauni milioni 59.2.
Kwa upande wao, matajiri wa Man City wameripotiwa kutenga kitita cha Pauni milioni 70 kumng’oa Livramento katika kikosi cha Newcastle.


