MADRID, Hispania
REKODI ya mkongwe Raul Gonzalez iliyodumu kwa miaka 30 katika klabu ya Real Madrid imevunjwa rasmi.
Ni katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya vigogo wa Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga), Bayern Munich.
Katika mechi hiyo, kocha wa Madrid, Alvaro Arbeloa, alimuanzisha Tiago Bitarsh na ‘dogo’ huyo akavunja rekodi ya Raul.
Bitarsh ana miaka 18 na siku 247, hivyo anakuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi baada ya Raul kuingia kikosi cha kwanza cha Madrid katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Kama haijasahaulika, Raul raia wa Hispania aliweka rekodi hiyo ya aina yake mwaka 1996.


