18.1 C
New York

Arsenal yakaribia kumnasa Diomande

Published:

LONDON, Uingereza

WASHIKA Bunduki wa London, Arsenal, wanapewa nafasi kubwa ya kumsajili mshambuliaji wa RB Leipzig ya Bundesliga, licha ya Liverpool nao kumtolea macho.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 19, alijiunga na Leipzig mwaka jana na ameshafunga mabao 11 na kutoa ‘asisti’ nane katika michezo yake 29.

Diomande raia wa Ivory Coast, pia anawaniwa na mabosi wa klabu za Manchester United na Barcelona.

Kwa mujibu wa mtandao wa CaughtOffside, Arsenal wana nafasi kubwa zaidi kwa kuwa wao wako tayari kuweka mezani Pauni milioni 89 wanazotaka Leipzig.

Liverpool wao wanaamini Diomande anatosha kuziba pengo la Mohamed Salah, ambaye ameshaweka wazi mpango wake wa kuondoka Anfield mwishoni mwa msimu huu wa 2025-26.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img