MANCHESTER, Uingereza
PEP Guardiola na vijana wake wa Manchester City wameandika historia ya aina yake baada ya ushindi wa mabao 4-0 walioupata dhidi ya Liverpool.
Erling Haaland alifunga ‘hat-trick’ na Antoine Semenyo kuongeza moja katika robo fainali hiyo ya Kombe la FA iliyochezwa katika Uwanja wa Etihad jijini Manchester.
Hiyo inakuwa mara ya nane mfululizo kwa Man City kuingia hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.
Wakati huo huo, Man City inakuwa timu ya kwanza kushinda mechi 18 mfululizo za nyumbani katika historia ya Kombe la FA.
Kwamba Man City wamevunja rekodi ya Clapham Rovers iliyokuwa na rekodi ya kushinda mechi 17 mfululizo za nyumbani kuanzia mwaka 1873 hadi mwaka 1881.


