18.1 C
New York

Kounde kutua City, Liverpool au Chelsea?

Published:

LONDON, Uingereza

KLABU za Manchester City, Liverpool na Chelsea zinapigana vikumbo kuiwania huduma ya beki wa Barcelona raia wa Ufaransa, Jules Kounde.

Kounde alitua Barcelona mwaka 2022 akitokea kwa wapinzani wao wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga), Sevilla.

Katika mechi 181 alizoshuka dimbani, nyota huyo amefunga mabao 10 na kutoa asisti 22.

Licha ya wimbi la majeraha, Kounde mwenye umri wa miaka 27 amekuwa na mchango mkubwa kwa Barcelona kila anapoingia kikosini.

Kwa msimu huu, mlinzi huyo amefunga mabao matatu na kutoa ‘asisti’ nne katika mechi 40 za mashindano mbalimbali.

Sasa, ripoti zinaeleza kuwa Man City, Liverpool na Chelsea zimeingia kwenye ushindani mkali wa kuifukuzia saini yake.

Taarifa zinaeleza kuwa Barcelona wao wako tayari kumwachia nyota huyo endapo watawekewa mezani kitita cha Pauni milioni 70.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img