18.1 C
New York

England ya Tuchel yachafua rekodi

Published:

LONDON, Uingereza

KWA mara ya kwanza katika historia, timu ya soka ya taifa ya England imepoteza mchezo mbele ya wapinzani kutoka Bara la Asia.

Ni baada ya vijana hao wa kocha Thomas Tuchel kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Japan katika mchezo wa kirafiki wa Machi 31, 2026 uliochezwa Wembley.

England sasa imebakiza mechi mbili pekee za ‘kutesti mitambo’ kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu.

Kwa upande mwingine, imekuwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 2024 kwa kipa wa England, Jordan Pickford, kuruhusu bao.

Ni mchezo ambao England walimaliza kipindi cha kwanza bila kupiga shuti lililolenga lango la Japan.

Hivyo, ni kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2017 kwa ‘Three Lions’ kukosa shuti lililolenga lango la wapinzani ndani ya kipindi chote cha dakika 45.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img