18.1 C
New York

Beki huyu kuziba pengo la Maguire

Published:

MANCHESTER, Uingereza

KLABU ya Manchester United imeanza kujipanga na maisha mapya bila mlinzi wake wa kati, Harry Maguire.

Ripoti zinaeleza kuwa Man United imejitosa kuiwania saini ya beki wa Toulouse ya Ufaransa, Charlie Cresswell.

Mbali ya beki, pia klabu hiyo imeripotiwa kuhitaji viungo wa kati wawili pindi dirisha kubwa litakapofunguliwa majira ya kiangazi.

Man United inaamini Maguire si beki wa kutegemewa kwa asilimia 100 kutokana na kiwango chake kupanda na kushuka.

Hivyo, anatakiwa beki mpya, hasa ikizingatiwa kuwa Matthijs de Ligt na Lisandro Martinez wamekuwa wakiandamwa na majeraha.

Ripoti zaidi zinaeleza kwamba Cresswell mwenye umri wa miaka 23 naye anavutiwa na tetesi za kutakiwa Old Trafford.

Hata hivyo, Man United watalazimika kuweka mezani kitita cha Pauni milioni 26 ili kuinasa saini yake.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img