5.7 C
New York

United yamtaka Tonali, yampotezea Guimaraes

Published:

MANCHESTER, Uingereza

KLABU ya Manchester United imeelekeza nguvu zake kwa Sandro Tonali na kuachana na staa mwenzake wa Newcastle United, Bruno Guimaraes.

Hata hivyo, kumshawishi Tonali kutategemea na uwezekano wa Man United kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Aidha, usajili wa Muitalia huyo unashinikizwa na kocha wa sasa, Michael Carrick, ambaye huenda akaajiriwa moja kwa moja hapo baadaye.

Taarifa za awali, kwa mujibu wa Gazeti la Daily Mail, zilieleza kuwa Man United inamtaka zaidi Guimaraes raia wa Brazil.

Lakini, ripoti mpya zinadai kuwa mabosi wa Old Trafford wameona ni bora kuelekeza nguvu zao kwa Tonali.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img