23.1 C
New York

Straika wa mabao 17 aibukia Arsenal

Published:

LONDON, Uingereza

ARSENAL wako mstari wa mbele katika mbio za kuinasa saini ya mshambuliaji tishio wa Ligi Kuu ya Ubelgiji, Nicolo Tresoldi.

Nyota huyo wa U-21 ya Ujerumani ameshaingia kambani mara 17 na kutoa ‘asisti’ tano katika mechi 48 za mashindano mbalimbali msimu huu.

Itakumbukwa kuwa Tresoldi alifunga moja katika sare ya mabao 3-3 dhidi ya Barcelona, kabla ya ‘kutupia’ tena walipokutana na Atletico Madrid.

Kabla ya mapumziko ya kalenda ya FIFA yanayoendelea kwa mechi za kimataifa, alikuwa amepachika mabao saba katika mechi saba mfululizo za Ligi Kuu.

Katika majukumu ya timu ya taifa, Tresoldi amefunga mabao 12 katika mechi 23 alizocheza akiwa na U-21 ya Ujerumani.

Nyota huyo mwenye asili ya Italia na Argentina, ana mkataba na Club Brugge utakaomalizika mwaka 2029.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img