CATALUNYA, Hispania
MABOSI wa Barcelona wamempa sharti la kukubali kupunguziwa mshahara mshambuliaji wao raia wa Poland, Robert Lewandowski.
Ofa waliyofika nayo mezani kwake ni ya mkataba wa mwaka mmoja, ambayo pia ina punguzo la asilimia 50 ya mshahara wake wa sasa.
Barcelona wako kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) kwa tofauti ya pointi nne na tayari wametinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Wacatalunya hao watakwaana na wenzao wa La Liga, Atletico Madrid, katika hatua hiyo ya robo fainali.
Lewandowski (37), ana mkataba na Barcelona utakaofikia ukomo mwishoni mwa msimu huu.
Licha ya idadi ndogo ya mechi 21 pekee alizocheza kutokana na majeraha, straika huyo amefunga mabao 16.


