10.1 C
New York

Huyu ndiye Katibu Mkuu mpya CAF, aanza na rekodi

Published:

CAIRO, Misri

SAMSON Adamu raia wa Nigeria ndiye aliyeteuliwa kukalia kwa muda kiti cha Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Uteuzi wake ndani ya Shirikisho hilo lenye makao makuu yake mjini Cairo, Misri umekuja baada ya nafasi hiyo kuachwa na Veron Mosengo-Omba aliyetangaza kujiuzulu.

Kwa upande mwingine, Adamu ameandika historia ya ain yake ya kuwa raia wa kwanza wa Nigeria kushika nafasi hiyo ndani ya CAF.

Katika taarifa yake kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter), Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) limempongeza Adam kwa kuandika historia hiyo.

“Pongezi nyingi kwa Samson Adamu wetu kwa kuteuliwa kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa CAF,” imeeleza taarifa ya NFF.

Kabla ya kushika wadhifa huo, Adamu alikuwa Mkurugenzi wa Mashindano wa CAF. Alichangia mafanikio makubwa ya fainali za AFCON, Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img