MANCHESTER, Uingereza µ
BARCELONA iko tayari kukaa mezani na Manchester United na kujadili dili la mshambuliaji raia wa Hispania, Ferran Torres.
Torres aliyewahi kukipiga Manchester City, amechangia mabao 60 na asisti 21 katika mechi 198 alizocheza akiwa Barcelona.
Mkataba wake utafikia ukomo mwaka 2027 na Barcelona wako tayari kumuuza mwishoni mwa msimu huu.
Ripoti zinaeleza kuwa Barca wanataka Man United imchukue Torres ili wao wabaki na Marcus Rashford. Katika hatua nyingine, klabu za Atletico Madrid na Juventus nazo zimetajwa kumtolea macho mshambuliaji huyo


