RIO, Brazil
MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Raphinha, amerejea klabuni hapo akitokea katika kambi ya timu ya taifa ya Brazil.
Raphinha amelazimika kurejea Barcelona kwa ajili ya matibabu baada ya kupata majeraha ya misuli akiwa na timu yake ya taifa.
Majeraha hayo ndiyo yaliyosababisha mchezaji huyo kutolewa mapema wakati Brazil ikifungwa mabao 2-1 na Ufaransa hivi karibuni.
”Raphinha alicheza vizuri sana lakini alipata majeraha mwishoni mwa kipindi cha kwanza, hivyo tukamtoa …” amesema kocha wa Brazil, Carlo Ancelotti.
Barcelona wana hofu kwa huenda Raphinha akarudiwa na majeraha ya misuli yaliyowahi kumuweka nje kwa miezi miwili.


