MADRID, Hispania
HAKUNA kitu kama hicho. Staa wa Real Madrid, Vinicius Jr, amepuuzia ripoti zinazodai kuwa ataondoka klabuni hapo.
Vinicius alikuwa kwenye wakati mbaya chini ya kocha aliyepita, Xabi Alonso, hivyo zikawepo tetesi kuwa angeondoka mwishoni mwa msimu huu.
Hata hivyo, kwa sasa Mbrazil huyo ni mchezaji muhimu kikosini, ambapo ameshafunga mabao 11 na ‘asisti’ mbili.
Akizungumza akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa ya Brazil, Vinicius amesema mpango wake ni kubaki Santiago Bernabeu.
“Ninachofikiria ni Real Madrid tu, kubaki hapo kwa muda mrefu zaidi,” amesema.
Wakati huo huo, Vinius alikanusha taarifa zinazomuhusisha na klabu za Ligi Kuu ya Marekani (MLS).


