MANCHESTER, Uingereza
ANAONDOKA au anabaki? Beki wa kati wa Manchester United, Harry Maguire, amefunguka juu ya hatima yake klabuni hapo.
Mlinzi huyo wa kimataifa wa England amefichua kuwa atasaini mkataba mpya hivi karibuni.
Mkataba wake wa sasa na mabingwa hao mara 20 wa taji la Ligi Kuu ya England utafikia ukomo mwishoni mwa msimu huu.
Maguire (33), amekuwa na kiwango bora chini ya kocha wa muda wa kikosi hicho, Michael Carrick.
Kutokana na uwezo mkubwa huo, beki huyo wa zamani wa Leicester City ameweza kurejesha nafasi yake katika kikosi cha timu ya taifa ya England.
“Nafikiri mazungumzo yanaendelea. Nadhani tutafikia pazuri kwa masilahi yangu na klabu,” amesema.


