9.5 C
New York

Yanga v Simba; ‘Kariakoo Derby’ ya maswali mengi ndani ya uwanja

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

YANGA itakuwa mwenyeji wa mchezo kuwakaribisha wapinzani wao, Simba, katika dakika 90 za mtoto, ukiwa ni mwendelezo wa Ligi Kuu Bara msimu huu wa 2025-26.

Huku kila moja ikiwa imeshashuka dimbani mara 10, Yanga wako kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 28. Ni baada ya ushindi wa mechi tisa kati na sare moja.

Kwa upande wao, Simba wamekusanya pointi 23 baada ya kushinda saba, sare mbili na kufungwa mechi moja.

Aidha, ‘Wananchi’ watashuka dimbani wakiwa na kasi ya kupoteza mechi moja pekee kati ya tano zilizopita, ikishinda tatu na kutoa sare moja.

Je, Simba watauzima moto huo wa vijana wa Pedro, ambao hawajafungwa katika mechi tatu mfululizo? Hilo ni swali la kwanza.

Kwa upande wao, Wekundu wa Msimbazi hawajafungwa katika michezo mitano ya hivi karibuni, na badala yake wameshinda mitatu na kutoa sare mbili.

Je, baada ya kulazimishwa suluhu (0-0) na Dodoma Jiji, Simba watarejesha kasi yao ya awali, ambapo walikuwa wameshinda mara tatu mfululizo kabla ya mchezo huo? Hilo ni swali la pili.

Safu ya ushambuliaji ya Yanga iko kwenye kiwango kizuri, ambapo imefunga mabao 11 katika mechi tano za hivi karibuni. Ni wastani wa mabao mawili kila mchezo.

Wakati huo huo, safari hii wanakutana na ‘ukuta’ (safu ya ulinzi) wa Simba, ambayo imeruhusu bao moja pekee katika michezo mitano iliyopita.

Je, nani kutamba Marchi Mosi? Ni ukuta wa Simba au safu ya ushambuliaji ya Yanga? Hilo ni swali la tatu linalosubiri majibu.

Eneo la ushambuliaji la Simba halijawa kwenye kiwango bora msimu huu. Wana mabao sita tu ya kufunga katika mechi tano zilizopita. Je, makali yao yataanzia kwa Yanga? Hilo ni swali la nne.

Simba wataingia uwanjani wakiwa na rekodi mbovu katika mechi zao za ‘derby’ dhidi ya Yanga. Haijashinda hata mechi moja kati ya tano zilizopita.

Katika mechi hizo, Simba imefungwa zote kwa jumla ya mabao 7-1. Je, safari hii Wekundu wa Msimbazi watazinduka na kupata ushindi? Hilo ni swali la tano.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img