9 C
New York

Waziri Mkuu Pakistan hali mbaya gerezani

Published:

ISLAMABAD, Pakistan

WAZIRI Mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan, anaelekea kupoteza uwezo wake wa kuona, wakati huu akiendelea kutumikia kifungo cha gerezani.

Khan, ambaye alishika wadhifa huo kuanzia mwaka 2018 hadi 2022, alihukumiwa mwaka 2023 baada ya kukutwa na hatia katika mashitaka takribani 100, yakiwamo ya kujihusisha na rushwa.

Sasa, akiwa bado gerezani, taarifa zinadai kuwa jicho lake la kulia limeooteza asilimia 15 ya uwezo wake wa kuona.

Kwa mujibu wa mwanasheria wake, Salman Safdar, jicho limefikia hatua hiyo kutokana na uzembe na makusudi ya mamlaka za gerezani.

Kwamba Khan hakuwa akipewa huduma makini, licha ya kwamba alishafikisha changamoto yake ya kusumbuliwa na jicho.

Safdar ameeleza kuwa Khan, ambaye aliwahi kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Kriketi ya Pakistan, alianza kupata shida hiyo miezi minne iliyopita.

“Licha ya kuiambia mamlaka ya gerezani, hakuna alichosaidiwa zaidi ya kupewa dawa ya maji ya kunyunyuziwa jichoni,” amesema Safdar.

Hata hivyo, Serikali ya Pakistan imeibuka na kukanusha taarifa za Waziri Mkuu huyo wa zamani kutokupewa huduma za afya kipindi hiki akiwa gerezani.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img