9 C
New York

Kim amteua binti yake kuwa mrithi

Published:

SEOUL, Korea Kaskazini

RAIS wa Korea ya Kaskazini, Kim Jong Un, ameripotiwa kumteua binti yake kuwa mrithi wake katika siku za usoni.

Binti huyo, Kim Ju Ae, ameonekana kuwa karibu na baba yake katika picha za hivi karibuni, ikiwamo wakati wa ziara ya Beijing, China, iliyofanyika Septemba, 2025.

Kwa mujibu wa Mbunge Lee Seong-kwen, binti huyo ameshapewa mafunzo ya kuandaliwa kuwa mrithi wa Kim.

Wengi wanasubiri kuona kama Ju Ae atahudhuria Mkutano Mkuu wa Chama tawala cha Korea ya Kaskazini utakaofanyika Februari hii.

Mbali ya mambo mengine, Mkutano huo unaofanyika mara moja kila baada ya miaka mitano hujadili sera za kimataifa, mipango ya kivita na mikakati ya nyuklia.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img