13.9 C
New York

Polisi washikilia watu sita maandamano Italia

Published:

MILAN, Italia

IMERIPOTIWA kuwa watu sita wako kwenye mikono ya polisi katika maandamano ya kupinga michuano ya Olimpiki mjini Milan.

Milan ni moja ya miji sita ya Italia itakayotumika kwa ajili ya michuano hiyo ya kipindi hiki cha majira ya baridi.

Hata hivyo, maelfu ya raia wa Italia wameingia barabarani wakitaka mashindano hayo yasifanyike kwa kuwa nchi hiyo inapitia hali ngumu ya kiuchumi.

Wananchi hao wameonekana wakiwarushia mawe polisi. Katika picha na video zilizosambaa, vyombo vya dola vinatumia maji ya kuwasha kujaribu kuwatuliza waandamanaji.

Hiyo ni kwa upande wa Milan, lakini maandamano ya Mji wa Turin yameshuhudia polisi zaidi ya 100 wakijeruhiwa na raia.

Wakati huo huo, Serikali imeeleza kuwa inaendelea kuchunguza waliohusika katika uharibifu wa miundombinu ya usafiri wa treni.

Naye Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni, amewaita kuwa ni ‘maadui’ wa nchi hiyo wale wote wanaopinga Olimpiki kufanyika.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img