13.9 C
New York

Madrid yamkomalia Rodri

Published:

MADRID, Hispania

KLABU ya Real Madrid imerejea kwa kasi katika mpango wake wa kumfukuzia kiungo wa Manchester City na timu ya taifa ya Hispania, Rodri Cascante.

Wanachokiona mabosi wa Madrid ni kwamba kikosi chao kinakosa kiongozi ndani ya uwanja tangu Sergio Ramos, Casemiro, Toni Kroos na Luka Modric walioondoka.

Taifa zinaeleza kuwa kuondoka kwa kocha Xabi Alonso ulikuwa ni mpango wa kwanza wa Rais Florentino Perez kufanya mabadiliko makubwa kikosini.

Na sasa, tajiri huyo wa Santiago Berabeu anapambana kuinasa huduma ya Rodri, ambaye hatima yake katika klabu ya Man City haijaeleweka.

Kwa sasa, nyota huyo amebakiza miezi isiyozidi nane katika mkataba wake na Madrid, huku ikielezwa kuwa hakuna mazungumzo ya kupewa mwingine.

Rodri, mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or kwa mwaka 2024, amewahi kukiri kuwa aliwahi kufikiria kujiunga na Madrid wakati fulani wa maisha yake ya soka.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img