LONDON, Uingereza
CHELSEA iko njiani kuachana na beki wake wa kati raia wa Ufaransa, Benoit Badiashile. Ataondoka klabuni hapo majira ya kiangazi ya mwishoni mwa msimu huu wa 2025-26.
Badiashile amejikuta kwenye wakati mgumu kupata namba tangu kocha Liam Rosenior alipotua Stamford Bridge. Amecheza mara sita katika mechi nane za Muingereza huyo.
Ripoti zinaeleza kuwa kwa sasa nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 anazigonganisha klabu za Serie A na Ligue 1, ambazo ni AC Milan, Juventus na Marseille.
Hata hivyo, bado Blues hawajaweka wazi kuwa wako tayari kumwachia mlinzi huyo mara tu msimu huu utakapofikia ukomo.
Na endapo italazimika kumuuza, basi Blues itahitaji si chini ya Pauni milioni 30.4 kutoka kwa klabu itakayomtaka mchezaji huyo.


