10.7 C
New York

Alcaraz alivyoweka rekodi tenesi duniani

Published:

MADRID, Hispania

BAADA ya kumfunga mkongwe Nikovac Djokovic, Carlos Alcaraz ameandika historia mpya katika mchezo wa tenesi duniani.

Alcaraz raia wa Hispania, alimtandika Djokovic na kutwaa ubingwa wa michuano ya Australian Open wikiendi iliyopita (Februari Mosi, 2026).

Kwa ushindi huo, anakuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi, miaka 22, kubeba mataji yote makubwa manne (Australian Open, French Open, Wimbledon na US Open).

Kabla ya ubingwa wa Jumapili, Alcaraz hakuwahi kufika walau nusu fainali ya Australian Open. Aliishia robo fainali mara zote nne alizokuwa ameshiriki.

“Kila nilipokuja Asutralia, nilikuwa nikifiria kuhusu kuwa bingwa lakini haikutokea. Mwaka huu, nilikuja nikiwa na kiu zaidi. Ndoto yangu imetimia,” amesema Alcaraz.

Katika historia ya tenesi, aliyekuwa akishikilia rekodi hiyo ni Don Budge, ambaye alitwaa mataji hayo akiwa na umri wa miaka 22 na siku 355 mwaka 1938.

Wakati huo huo, Alcaraz anafikisha taji lake kubwa la saba, licha kwamba alianza tenesi miaka sita tu iliyopita.

Ni kwa maana hiyo, anaungana na Djokovic, Rafael Nadal, Roger Federer, Andre Agassi na Rod Laver na kuwa mchezaji wa sita kuwahi kutwaa mataji yote makubwa manne ya mchezo wa tenesi.

Lakini, historia inatukumbusha kuwa Alcaraz anakuwa mchezaji wa kwanza tangu Djokovic alipofanya hivyo mwaka 2016.

Hata hivyo, kwa upande wa wanaume, Djokovic alikuwa na taji kubwa moja tu kabla ya kufikisha umri wa miaka 23.

Aidha, kwa umri wake wa miaka 22, anakuwa mchezaji mdogo zaidi kuwa bingwa wa mashindano makubwa, akiipiku rekodi ya Nadal, ambaye alifanya hivyo akiwa na miaka 24 mwaka 2010.

Safari yake ya kubeba mataji haikuwa rahisi kwani mara zote nne amecheza fainali dhidi ya wachezaji wakubwa kwenye tenesi.

Ukiweka kando Djokovic, ambaye amewafunga Jannik Sinner (mara mbili), Alexander Zverev na Casper Ruud.

Djokovic amezungumzia kiwango bora cha Alcaraz akisema: “Matokeo (dhidi yangu) ni ushahidi tosha wa kiwango bora alichonacho kwa sasa. Anastahili sifa zote anazopewa.”

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img