10.5 C
New York

Kiongozi Boko Haram auawa

Published:

LAGOS, Nigeria

JESHI nchini Nigeria limefanikiwa kumuua aliyekuwa kiongozi wa Kundi la kigaidi la Boko Haram, Abu Khalid, katika operesheni iliyofanyika katika Msitu wa Sambisa huko Kaskazini-Mashariki mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Nigeria (NAN), Khalid alikuwa kiongozi wa pili kimamlaka na mwenye ushawishi mkubwa katika Kundi hilo la waasi.

Taarifa zaidi zinamtaja kuwa ndiye aliyekuwa akiratibu na kusimamia operesheni za Boko Haram, hasa katika matukio yao ya utekaji na mashambulizi.

Hivyo, kuuawa kwake kunatajwa kuwa ni hasara kwa Boko Haram na kutaathiri kwa kiasi kikubwa mikakati yake.

Kwa upande wake, jeshi la Nigeria limesema kuuawa kwa Khalid ni moja ya mafanikio ya operesheni za kutokomeza ugaidi na vikundi vya uasi nchini humo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img