JERUSALEM, Palestina
WANAJESHI wa Israel wameua jumla ya raia wa Palestina wanaotajwa kufikia 32 katika mashambulizi yao ya wiki chache za hivi karibuni.
Taarifa hiyo imeelezwa na Wizara ya Afya ya Palestina katika taarifa yake ya leo Februari Mosi, 2026.
Bado kumekuwapo kwa mapigano kati ya vikosi vya Marekani na wapiganaji wa Palestina, Hamas, licha ya jitihada kubwa zinazofanywa na Marekani katika kutafuta suluhu.
Licha ya pande mbili hizo kukaa mezani na kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano, kila mmoja amekuwa akimshutumu mwenzake kwa kukiuka yale yaliyofikiwa.
Israel imeendelea kushambulia maeneo ya Ukanda wa Gaza, likiwamo shambulizi lililosambaratisha kituo cha polisi na nyumba za Serikali.
“Idadi ya vifo imeongezeka, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto,” amesema Msemaji wa Wizara ya Afya ya Polisi, Mahmud Bassal.


