11.2 C
New York

Arsenal yafikia rekodi ya Man United, Chelsea

Published:

LONDON, Uingereza

USHINDI wa mabao 4-0 dhidi ya Leeds United umeifanya Arsenal kuifikia rekodi iliyodumu kwa miaka 26 katika michuano ya Ligi Kuu ya England (EPL).

Ushindi huo umetokana na mabao ya Martin Zubimendi, Viktor Gyokeres, Gabriel Jesus na Karl Darlow aliyejifunga.

Washika Bunduki hao wa London walishuka dimbani wakiwa na machungu ya kukosa ushindi katika michezo mitatu mfululizo.

Kabla ya kuivaa Leeds, vijana hao wa kocha Mikel Arteta walitoa sare mara mbili dhidi ya Liverpool na Nottingham Forest, kabla ya kufungwa mabao 3-2 na Manchester United.

Kwa kuifunga Leeds, Arsenal inakuwa timu pekee baada ya Man United na Chelsea kufunga mabao manne ugenini katika mechi tano tofauti dhidi ya mpinzani mmoja.

Chelsea wana historia ya kuwafanyia hivyo majirani zao wa London, Tottenham, wakati Man United waliifunga Bolton Wanderers.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img