11.2 C
New York

Mourinho apewa Madrid

Published:

NYON, Uswis

HATIMAYE Droo ya mechi za ‘play off’ za kusaka tiketi ya kucheza hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imechezeshwa leo Januari 30, 2026 mjini Nyon, Uswis.

Timu zilizoshika nafasi ya tisa hadi ya 24 kwenye msimamo wa Ligi ya Mabingwa ndizo zilizokutanishwa, hivyo kupatikana mechi nane za play off.

Ikumbukwe, tayari Arsenal, Bayern Munich, Liverpool, Tottenham, Barcelona, Chelsea, Sporting Lisbon na Manchester City zilishaingia 16 Bora.

Mechi za play off, kwa mujibu wa ratiba ya Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA), zitaanzwa kuchezwa Februari 17, mwaka huu.

Sasa, kwa droo ya leo, kivutio kikubwa ni mechi kati ya vigogo wa soka la Ureno, Benfica, na wakali wa La Liga, Real Madrid.

Mvuto wa mchezo huo ni kwamba Benfica inanolewa na Jose Mourinho, hivyo kocha huyo atakuana na Madrid, ambao ni mabosi wake wa zamani.

Mechi zingine ni kama ifuatavyo; Bodo/Glimt v Inter Milan, Monaco v PSG, Qarabag v Newcastle United, Galatasaray v Juventus.

Wakati huo huo, kuna michezo hii; Club Brugge v Atletico Madrid, Borussia Dortmund v Atalanta, na Olympiacos v Bayer Leverkusen.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img