11.2 C
New York

Grealish nje hadi msimu ujao

Published:

MERSEYSIDE, England

NI pigo kwa Jack Grealish, ambapo mshambuliaji huyo wa Everton atalazimika kuwa nje ya uwanja kwa kipindi chote cha msimu huu.

Grealish anayecheza kwa mkopo akitokea Manchester City, anasumbuliwa na majeraha ya mguu na anatarajiwa kufanyiwa upasuaji.

Nyota huyo wa kimataifa wa England alipata majeraha hayo Januari 18, 2026, siku ambayo alikuwa uwanjani kuikabili Aston Villa.

Aliyethibitisha kuwa Greliash hatarejea hadi msimu ujao ni kocha wake, David Moyes. “Tunaamini anahitaji upasuaji …” amesema.

Baada ya kuondoka Man City akionekana amekwisha, Grealish ameweza kurejesha makali yake tangu alipotua kwa mkopo Everton.

Kabla ya majeraha, tayari alishapachika mabao mawili na kutoa ‘asisti’ sita katika michezo 22 aliyocheza msimu huu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img