8.4 C
New York

Polisi wakanusha waasi kuvamia kanisa

Published:

LAGOS, Nigeria

POLISI nchini Nigeria wamekanusha taarifa zinazodai kuwa kikundi cha waasi kimevamia kanisa na kuteka waumini huko maeneo ya Kaskazini.

Akikanusha uvumi huo, Kamishna wa Polisi wa Jimbo la Kaduna,  Alhaji Muhammad Rabiu, amesema taarifa hizo hazina ukweli, na badala yake zimelenga kuchochea machafu.

Kamishina huyo ameenda mbali zaidi na kusema kama kuna anayeweza kuthibitisha kutokea kwa hilo, basi ajitokeze na kutaka majina ya watu waliotekwa.

Kwa miaka ya hivi karibuni, hali ya usalama nchini Nigeria imekuwa ikiyumbishwa na matukio ya uvamizi na utekaji katika makanisa na misikiti.

Katika matukio mengi, watekaji hao wamekuwa wakiwashikilia waumini kwa shinikizo la kutaka kulipwa kiasi cha fedha.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img