MILAN, Italia
KLABU ya Inter Milan imeanza harakati za kuinasa saini ya mlinda mlango wa Aston Villa na timu ya taifa ya Argentina, Emi Martinez.
Inter imemuweka Martinez kwenye rada zake ili akazibe pengo la Yann Sommer kwa ajili ya mashindano ya msimu ujao wa 2026-27.
Hata hivyo, Martinez atalazimika kukubali kupunguza mshahara wake ili klabu hiyo ya Serie A iweze kumudu usajili wake.
Martinez, kipa wa zamani wa Arsenal mwenye umri wa miaka 33, bado ana mkataba mrefu na Villa, ambao utafikia ukomo wake mwaka 2029.
Wakati wa usajili wa kiangazi, mwaka jana, Manchester United ilijaribu kumsajili lakini ilishindikana na ndipo ikamchukua Senne Lammens.


