10.5 C
New York

Kovac atajwa kibarua Man United

Published:

MANCHESTER, Uingereza

JINA la Niko Kovac limeingia rasmi katika orodha ya makocha wanaohusishwa na kibarua cha kuinoa Manchester United msimu ujao.

Taarifa rasmi zinaeleza kuwa kocha huyo wa Borussia Dortmund ya Bundesliga naye anavutiwa kupewa majukumu hayo pale Old Trafford.

Benchi la ufundi la ‘Mashetani Wekundu’ lipo chini ya kiungo wao wa zamani, Michael Carrick, ambaye atakuwa hapo hadi mwishoni mwa msimu huu.

Itakumbukwa, Man United waliachana na Ruben Amorim mwezi uliopita akiwa amehudumu klabuni hapo kwa miezi 18 pekee.

Wakati jina la Kovac likiibuka, bado pia Man United imeendelea kuhusishwa na Thomas Tuchel anayeinoa timu ya taifa ya England na kocha wa Marseille, Roberto De Zerbi.

Kovac, raia wa Croatia mwenye umri wa miaka 54, anakaribia kutimiza mwaka mmoja tangu alipokabidhiwa majukumu ya kuinoa Dortmund.

Kwa nyakati tofauti, mchezaji huyo wa zamani amezinoa Bayern Munich, Eintracht Frankfurt, Wolfsburg, Monaco na timu ya taifa ya Croatia.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img